Discussion

...................................................

...................................................

...................................................

...................................................

kibongobongo mpango mzima

kibongobongo mpango mzima

HII NDIYO LAANA YA WAZAZI INAYOMNYEMELEA PRODUCER LUCCI

Posted in
No comments
Wednesday, May 28, 2014 By Unknown

Lucci akiwa na Lisa

Mtaarishaji wa Muziki katika studio za Transfomax Lucci ananyemelewa na laana ya wazazi iwapo atafunga ndoa mwezi wa sita mwaka huu, chanzo cha habari cha gazeti la makorokocho kutokana kwenye ukoo mmoja wa Producer Luciano Tsere a.k.a Lucci kinadai kuwa Producer huyo yuko kwenye mipango kabambe ya kufunga ndoa na mwanadada Lisa Stevens aliyezaa nae mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Lee Roy na ndoa hiyo eti imepangwa kufanyika mwezi wa sita wakati familia inataka ijipange mpaka Baba yake Lucci arudi nchini kutoka Malawi ambako anaiwakilisha Tanzania kama balozi na inasemekana Balozi Tsere hawezi kurudi nchini kipindi hiki kwasababu Malawi wako katika mchakato wa uchaguzi mkuu wa Rais, sasa Lucci amechomoa kuingia kwenye ratiba ya kifamilia badala yake eti baada ya kususiwa harusi na familia ameamua kuwaalika kati bata la harusi washkaji zake wa karibu wachache pamoja na ndugu wa Lisa wachache, sasa ndo tusubiri siku zifike halafu tuone, ila inasemekana mipango ya ndoa kwa Upande wa Lucci imekamilika full full, na kumbuka kwamba Lucci alishamvalisha pete Lisa. 
Tunavyofahamu kwa mila na desturi za kiafrika kwa yeyote anakwenda kinyume na makubaliano na wazazi wake hupata Laana.
Nilipompigia simu Lucci na kumuuliza juu ya msala huu, alionesha kushtushwa kidogo na kudadisi nimezipata wapi taarifa hizi za ndani ya familia yao, akaji ng'atang'ata kisha akadai uko katika kikao kizito hivyo nimpigie baade. 

 Siku Lucci alipomvisha pete ya Uchumba Lisa.

Related posts

0 comments:

About the Author

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Pellentesque volutpat volutpat nibh nec posuere. Donec auctor arcut pretium consequat.

Proudly Powered by Blogger.