Discussion

...................................................

...................................................

...................................................

...................................................

kibongobongo mpango mzima

kibongobongo mpango mzima

MAZUNGUMZO YA SUDAN-K BADO KIZUNGUMKUTI.

Posted in
No comments
Tuesday, June 17, 2014 By Unknown

Rais Salva Kiir anataka kuombwa msamaha kwa kutusiwa na Balozi Mahboub
Awamu mpya ya mazungumzo yanayolenga kumaliza mapigano ya miezi sita nchini Sudan Kusini imeahirishwa mara moja baada ya serikali na waasi kutoa masharti mapya. Hatua hiyo inajiri wiki moja tu baada ya Rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar kukubaliana kubuni serikali ya mpito katika kipindi cha miezi miwili ijayo.
MKuu wa ujumbe huo Michael Makuei amesema kuwa wanangojea msamaha kutoka kwa bodi inayosimamia mazungumzo hayo,IGAD na Balozi Mahboub Maalim aliyemwita Rais Salva Kiir Mjinga.
Katika kizazaa kinachozunguka mazungumzo hayo ,ujumbe wa serikali ulijitoa katika mazungumzo hayo ili kupinga kile walichokitaja kuwa matamshi machafu dhidi ya rais salva kiir na maafisa wanaosimamia mazungumzo hayo.
Kwa upande mwengine waasi nao wanataka pande zaidi kuhusishwa katika mazungumzo hayo wakiwemo wafungwa wa zamani pamoja na viongozi wa dini. Viongozi wa eneo hili wametishia kuziwekea vikwazo pande pinzani katika mazungumzo hayo iwapo zitashindwa kuafikiana kisiasa. Maelfu ya watu wamefariki huku zaidi ya watu milioni moja wakitoroka makaazi yao tangu vita hivyo vianze mnamo mwezi Disemba. Kwa sasa mashirika ya misaada yameonya kuzuka kwa baa la njaa.

Related posts

0 comments:

About the Author

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Pellentesque volutpat volutpat nibh nec posuere. Donec auctor arcut pretium consequat.

Proudly Powered by Blogger.