Discussion

...................................................

...................................................

...................................................

...................................................

kibongobongo mpango mzima

kibongobongo mpango mzima

MFANYABIASHARA MWENYE JAMII YA ASIA APIGWA RISASI NA KUFARIKI HAPOHAPO NA MAJAMBAZI HUKO KARIAKOO, DAR ES SALAAM

Posted in
No comments
Thursday, January 16, 2014 By Unknown

Tukio hilo limeotokea Jumamosi majira ya saa 12 kasoro jioni limeelezwa kuwa aliyepigwa risasi na kufariki papo hapo ni Mfanyabiashara mmoja (Jina Halikufahamika) Mwenye asili ya Asia aliyeshambuliwa na majabazi watatu kwa kupigwa risasi katika paji la uso wake na kisha majambazi hao kutoweka na mabegi mawili yaliyoojaa fedha.
Damu ya Mfanyabiashara huyo ikiwa imetapakaa katika gari lake baada ya kupigwa risasi na majambazi waliompora kiasi kikubwa cha fedha na kutoweka.

Wakielezea tukio hilo baadhi ya wafanyabiashara wengine katika maeneo hayo ya mtaa wa Lindi na Kongo (Kariakoo) walidai kwamba Mfanyabiashara huyo alitoka na kufunga duka lake huku akiwa na mabegi mawili na Mashine ya kutolea Risiti ya EFD na kuelekea katika gari lake dogo aina ya Suzuki Carry na Ghafla walitokea watu wawili waliokuwa katika pikipiki na mmoja wa tatu alikuwa amesimama pembeni kidogo na gari hiyo na kisha kuelekea moja kwa moja katika gari hiyo na kumpiga risasi mfanya biashara huyo aliyekuwa akijiandaa kuondosha gari lake.
Watu mbalimbali katika eneo la tukio Kariakoo wakishangaa kilichotokea.

Hata hivyo haikujulikana kwa haraka ni kiasi gani cha fedha ambacho kilikuwemo katika mabegi hayo. Wakiongea na mwandishi wetu baadhi ya mashuhuda wa tukio walidai kuwa majambazi hao walikuwa  watatu na mmoja alikuwa na bunduki aina ya SMG

Hata hivyo baadhi ya watu wamelaumu utaratibu wa wafanya biashara wengi wa kariakoo kuhifadhi fedha nyingi katika maduka na badala yake wamewataka wafanya biashara hao kutafuta mbinu mbadala itakayowaezesha kuweka fedha na mali zao salama.
 
 Pamoja na kutumia huduma za kuhamisha fedha kwa kutumia mitandao, cheque, na hata credit card kuliko Cash kwani imekuwa kawaida kwa mtukio haya kujirudia eleo hili la Kariakoo.

Related posts

0 comments:

About the Author

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Pellentesque volutpat volutpat nibh nec posuere. Donec auctor arcut pretium consequat.

Proudly Powered by Blogger.