HUYU NDIYE MREMBO ATAKAYEKUWA VIDEO QUEEN YA NYIMBO MPYA YA OMMY DIMPOZ ANAYOIFANYA HUKO LONDON.
Posted in
No comments
Saturday, March 29, 2014 By Unknown
Ommy Dimpoz amerudi Tanzania March 10, 2014 saa tano usiku ambapo AyoTV na millardayo.com ziliweza kumnasa baada ya kushuka kutoka katika ndege uwanja wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Amethibitisha ni kweli amefanya video yake mpya London ambapo aliehusika kama Director ni mshkaji ambae amefanya video kadhaa za wakubwa wa Afrika kama Azonto ya FUSE ODG, video za caro ya Wizkid na Davido ‘skelewu’.
Hizi zinazofata hapa chini ni baadhi ya picha za utengenezwaji wa video hiyo mpya ya Ommy Dimpoz huko London.
Huyu hapa chini ndio Director mwenyewe anaitwa Moe Musa Mwingereza mwenye asili ya Nigeria ambae unaambiwa gharama ya video anazozifanya ni kuanzia dola za kimarekani elfu 20 na kuendelea, kwa haraka haraka ni zaidi ya milioni 30.
Related posts
Share this post
0 comments: