ALIKIBA KUWA MFANO KWA WAASANII LIMBUKENI WA MAISHA
Posted in
No comments
Saturday, April 12, 2014 By Unknown
Wasanii wengi wa fani mbali mbali kuanzia filamu hadi bongo fleva, wamekuwa wakipoteza mashabiki wao wengi kutokana na ile hali tu ya jinsi anavyochukulia umaarufu wake, kama anatumia umaarufu wake vizuri basi hutokea kupendwa sana na watu hata wale ambao siyo mashabiki wake, watampenda tu kama mtu wakawaida.Kismati hiki cha kupendwa sana na watu wa rika mbalimbali anacho naye msanii mkongwe sana Ali Kiba.
Ukimuongelea Msanii kama Ali Kiba, watu wengi wanatamani wasanii wote wawe kama yeye,ni mmoja kati ya wasanii wachache sana maarufu ambao hawana ulimbukeni wa mali au umaarufu wao, cause wengi wao pale wapatapo umaarufu kidogo tu, huanza kudharau watu wake wa karibu, haswa wakipata mali kidogo basi huishia kuonyesha watu magari na
nyumba,hata kama haiwahusu, ilimradi tu basi nao waonekane kama wasanii wa nje wenye mali zao, ila kwa Ali kiba imekuwa ni tofauti sana,na hiki ndicho kinachofanya AliKiba aweze kupendwa zaidi na kila mtu.
Kupitia mtandao wa instagram Ali kiba aliweza kuweka wazi mtazamo wake wa mafanikio:
“Kuishi maisha halisi yenye furaha na maana kwako ni kitu cha thamani sana. Unayo kila sababu ya kufuata njia yako ya maisha yenye misingi mizuri ya kukujenga katika kila nyanja ya maisha yako. Kwa kuwa kila mtu ana maono yake binafsi kuhusu maisha ni vigumu kufafanua maana halisi ya maisha. Naamini nawe pia una falsafa yako ya kutafsiri nini maana ya maisha mazuri kwako,”
Related posts
Share this post
0 comments: