Discussion

...................................................

...................................................

...................................................

...................................................

kibongobongo mpango mzima

kibongobongo mpango mzima

JACKLINE WOLPER AZUNGUMZIA JUU YA KUBADILI DINI NA AGUSIA SUALA LA KUACHANA NA USAGAJI.

Posted in
No comments
Friday, May 9, 2014 By Unknown

Ni muda mrefu  kidogo  baada  mwigizaji Mtanzania Jaqueline Wolper kutosikika  akiyatoa ya moyoni kuhusu yote yaliyompata kwenye miezi iliyopita na kumfanya amiliki sana headlines za magazeti, blogs, website pia facebook na twitter huku wengi wakiwa na hamu ya kusikia akiyaongelea.

Kwenye Exclusive interview na mtangazaji Sporah wa The Sporah show, Jack amekanusha kwamba yeye ni msagaji japo mara kadhaa ameonekana akivaa kiume.

"Sasa hivi nimepunguza sana kuvaa nguo za kiume, wengi walikua wanahisi lakini sijawahi kufanya vitendo vya usagaji na wala sijawahi kushawishiwa na mtu anaejihusisha na vitendo hivyo, boyfriend wangu hana tatizo na mavazi ya kiume ninayovaa… hatujawahi kupangiana mavazi"  Alisema  Wolper  na  kuongeza:

"Sijaolewa na wala sijawahi kuolewa, nilishawahi kubadili dini kweli… ni vitu vinatokea na usimuhukumu mtu bila kumuuliza"
 
Sporah: Ni kweli kwamba ulikutana na mtu ana uwezo wa kifedha na kulikua kuna vitu unataka akununulie akasema hawezi kukufanyia mpaka ubadilishe dini ili upate hizo mali?
 
J Wolper: Sio hivyo, dini nilikuja kubadilisha wakati nimeshapata mali, nilibadilisha mwishoni kabisa baada ya huyu mwanaume kuja kwetu akitaka kunioa, alinipa mali na vitu vya thamani kabla ya sisi kukutana, unajua unaweza ukawa unachat na mtu mkapendana lakini hamjawahi kukutana… ni mzuri wa kukushawishi, unajua sio rahisi mtu akiwa mbali aweze kukushawishi mkapendana wakati yeye yuko mbali na wewe uko mbali, namsifia kwa uzuri wake… sio wa umbo wala sura bali ana roho nzuri na alinitreat vizuri mpaka nikaona huyu ni sahihi nikabadilisha dini
 
Sporah: Ulifikiria kwamba dini yako sio nzuri au?
J Wolper: Kwa utamaduni wetu sisi Afrika, Tanzania ninavyojua hata kwa mama yangu imetokea, Mwanamke lazima ufate dini ya Mwanaume wako
 
Sporah: Lakini alikua bado hajakuoa? 
J Wolper: Nilikua tayari nimeshajiona kama mke wake, ni mtu ambae alinipenda sana…
 
Sporah: Ulijichora na tatoo ya jina lake?
J Wolper: Kwa nini nichore jina la mtu kwenye mwili wangu, kwanza yeye ni Muislamu hapendi tatoo… nilibadili dini kwa mapenzi yangu mwenyewe kutokana na mtu niliekua nae na hawajui alivyonishawishi mpaka mimi nikabadili, sio kwa kulazimishwa….
 
Ninachojua mimi heshima ni kufuata dini ya Mwanaume ukishachumbiwa, haikua kama girlfriend na boyfriend… alikua ananifanya kama mke wake japo hatukua tumekutana
 
Sporah: Ulijisikiaje pale vitu havikwenda vizuri?
J Wolper: Mi naona ni sawa tu kwa sababu Mungu pia anapanga ila sikuumia sana, ningeumia kama mimi ndio ningekua nimetaka kuolewa ila yeye ndio alitaka ndoa, mimi bado mdogo… watu wa mitandao kwao ni big deal ila kwangu sio kitu
 
Haukuwa uamuzi mgumu, napenda sana kufata moyo wangu… siwezi kufata moyo wa mtu, wengi waliniambia sijui ukibadili dini tena sijui mashabiki wako sijui nini nini… NOOOO! sio kuhusu mashabiki, mimi ni mimi kama mimi sikupenda kilichotokea na bado niko chini ya wazazi wangu, vp ikitokea nimekufa nitazikwaje sijaolewa??! mi siwezi kumchezea Mungu ndio maana ukiangalia instagram yangu mimi kila Jumapili lazima niende kanisani
 
J Wolper: Nilikaa miezi miwili bila kwenda Msikitini wala Kanisani, nilikonda kwa sababu siwezi kukaa bila kusali na wazazi wangu nakua nawakosea, kuna neno mama yangu mdogo aliniambia baada ya kukaa na mama na kuongea nikasema ngoja nirudi kanisani, siwezi kufaidisha watu na kuacha wazazi wangu wakasononeka… nilibadili dini kwa heshima ya mchumba wangu lakini sasa hivi nimerudi kwa heshima ya wazazi wangu
 
J Wolper: Bado Dallas ni rafiki yangu mkubwa sana kwangu na ni mtu poa, haongei mapenzi maskini… ni rafiki yangu ni kaka yangu, hatuwezi tena kuwa wapenzi… nampenda bado.
 
Interview nyingine ya Jackline iliyobaki unaweza kuitazama hapa chini…

Related posts

0 comments:

About the Author

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Pellentesque volutpat volutpat nibh nec posuere. Donec auctor arcut pretium consequat.

Proudly Powered by Blogger.