JE, WAJUA KUWA MTANDAO WA INSTAGRAM ULIMZUIA RIHANNA KUWEKA PICHA ZAKE KATIKA MTANDAO HUO
Posted in
No comments
Monday, May 12, 2014 By Unknown
Kwa Rihanna hua sio ‘big deal’ kupost picha za utupu katika mitandao ya kijamii, inavyoonekana ni moja ya starehe zake ambazo zimeonekana kuvuka mipaka iliyowekwa na wamiliki wa mtandao wa kushare picha wa Instagram.
Mwimbaji huyo wa Barbados, jana aliweka picha za utupu katika mtandao wa Instagram, lakini wamiliki wa mtandao huo waliziondoa picha hizo kwasababu zilikiuka masharti yanayozuia watumiaji kutoweka picha za aina hiyo katika mtandao huo.
Chanzo kiliuambia mtandao wa TMZ kuwa Instagram licha ya kuziondoa picha hizo pia walimtumia barua pepe ya kumuonya vinginevyo watamfungia kutoutumia mtandao huo. Hata hivyo Riri bado aliendelea kupost picha hizo katika mtandao wa Twitter.
Related posts
Share this post
0 comments: