Discussion

...................................................

...................................................

...................................................

...................................................

kibongobongo mpango mzima

kibongobongo mpango mzima

HILI NDILO NENO LA KWANZA LA DIAMOND BAADA YA KUSHINDWA KUNYAKUA TUZO ZA MTV AWARDS

Posted in
1 comment
Sunday, June 8, 2014 By Unknown

Capture

Macho na masikio ya Watanzania wengi kwa siku ya Jumamosi June 07 yote yalielekezwa Durban Afrika Kusini sehemu ambako zilikua zikitolewa tuzo za wateule wa MTV Afrika Music Award ‘MAMA’.

Furaha tuliyokuwa nayo Watanzania ilikua kubwa baada ya kuona kijana kutoka nyumbani Tanzania kuwa ni miongoni mwa vijana wanaochuana kwenye tuzo hizo tena akiwa vipengele viwili,ingawa bahati haikua njema kwa Diamond kwani hakufanikiwa kupata.

MOND22

Baada ya kutangazwa washindi hao na yeye kutokuwepo Dimaond Platnumz ameandika maneno haya kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii>’Maisha ni Hatua.. Nafkiri kwa mwaka huu ile ndio ilikuwa hatua yetu kwa MTV…Cha muhimu ni kujua wapi tulipokua mwaka jana na wapi tulipo leo… pia kujifunza na kujua ni nini cha kuongeza zaidi ili Next tym tuzidi kufanya vyema…. Shukrani zangu nyingi ziende kwa Mashabiki wote,Management, Media,Family, wasanii na wadau Mbalimbali kwani kwa nguvu zao ndio zimefanya leo kunisogeza toka sehem moja kwenda nyingine…Next stop #BET!!!… Asante sana #Sheriangoi kwa Suti Hii’.

Diamond Platnumz alikuwa pia ni moja kati ya watumbuizaji wa ugawaji wa tuzo hizi,ambapo kwa namna alivyoingia kwenye jukwaa na Davido  ilimfurahisha kila mtu aliyekuepo ukumbini na watu waliokuwa wakiangalia nyumbani kupitia DSTV.

Related posts

1 comment:

  1. Pamoja na hayo inabidi tusaport mziki wetu hasa mimi nawe sisi watanzania acheni maneno ya chinichini yasiyo na mwelekeo waowote wa maendeleo. kukosa ama kupata ni kanuni ya mchezo tu

    ReplyDelete

About the Author

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Pellentesque volutpat volutpat nibh nec posuere. Donec auctor arcut pretium consequat.

Proudly Powered by Blogger.