Discussion

...................................................

...................................................

...................................................

...................................................

kibongobongo mpango mzima

kibongobongo mpango mzima

PATA HABARI KAMILI JUU YA KIFO CHA MUONGOZAJI FILAMU BONGO, NDUGU GEORGE TYSON W MONALISA.

Posted in
No comments
Sunday, June 1, 2014 By Unknown

NI pigo tena kwa tasnia ya Bongo Muvi, mwongozi filamu Bongo na aliyekuwa mume wa staa wa filamu Bongo, Yvonny Cherry ‘Monalisa, George Tyson amefariki dunia baada ya kupata ajali mbaya ya gari eneo la Morogoro akitokea mkoani Dodoma. Tyson alikuwa ameambatana na watu kadhaa katika safari hiyo.
Marehemu Tyson akiwa na Monalisa (kushoto), kulia ni Tyson na mwanae Sonia.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Monalisa amemlilia Tyson kwa kuweka picha hiyo juu na kuandika maneno yafuatayo:

Monalisa akimnywesha kinywaji Tyson wakati wa kipaimara cha Sonia.

George Tyson enzi za uhai wake.


George Tyson akimlisha keki Yvonney Chery ‘Monalisa’ wakati mtoto wao Sonia alipopata kipaimara.




Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi.
Watu wawili wamepoteza maisha kutokana na ajali mbili zilizotokea  katika maeneo mawili tofauti na nyakati tofauti Mkoani Dodoma. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna

Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP ameeleza kuwa, ajali ya kwanza ilitokea tarehe 30/05/2014 majira ya saa 18:30hrs katika kijiji cha Ipala Wilaya ya Dodoma ambapo gari lenye namba za usajili DFP 614 Toyota Land Cruiser mali ya chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo likitokea chuoni kuelekea Dodoma mjini likiendeshwa na ALFRED S/O MLIGO, MIAKA 35, MHEHE, liliacha njia na kupinduka na kusababisha kifo chake.  Pia watu watano walipata maumivu mbalimbali na walitibiwa na kuruhusiwa.
 
Mwili wa marehemu upo katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma kusubiri taratibu nyingine.

Kamanda MISIME AMESEMA ajali ya pili imetokea majira ya saa 18:45hrs huko katika kijiji cha SILWA barabara ya Dodoma – Morogoro ambapo gari lenye namba za usajili T.150 CWA Toyota Granvia Station Wagon likiendeshwa na MGENI S/O SHEMAKAME, MBONDEI, MIAKA 29 MKAZI WA MBURAHATI DSM liliacha njia na kusababisha kifo cha GEORGE S/O TYSON, MIAKA 39, MWONGOZAJI WA FILAMU, Mkazi wa mbezi DSM. 

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Gairo ukisubiri taratibu za Polisi na wanandugu.
 
Pia katika ajali hiyo wanahabari wanne (4) wa Mboni show walipata majeraha mbalimbali na kutibiwa na kuruhusiwa, ambao ni:-

1.   NIXON S/O KABUMBILE, MHAYA, MIAKA 31
2.   GRACE D/O MEENA, MCHAGA, MIAKA 28
3.   NTWA S/O KABOLE, MNYAKYUSA, MIAKA 33
4.   JUSTINE S/O BAYO, MIAKA 27, MMASAI

Uchunguzi wa awali unaonyesha ajali zote mbili zimesababishwa na mwendokasi. Kamanda MISIME ametoa wito kwa madereva kuepuka mwendokasi na kuwa na udereva wa kujihami ambao unasaidia dereva kusimama bila kusababisha madhara linapotokea jambo lolote na hata kama ajali ikitokea madhara hayawezi kuwa makubwa kama yanavyokuwa anapokuwa kwenye mwendo wa kasi.



IMG_4162
Marehemu Geogre Tyson pichani hapa alikuwa yupo kijiji cha Chilonwa Chamwino kwenye utoaji wa madawati katika shule ya msingi Chaula iliyopo Dodoma. Baada ya kumaliza shughuli hii huku akiwa kama producer wa The Mboni Show mauti yalimkuta majira ya saa 12 jioni masaa 4 tu toka tuanze safari ya kurudi Dar es Salaam maeneo fulani hivi kama unataka kukaribia GAIRO mjini.
Katika gari hilo walikuwa watu 8 ila yeye pekee ndio aliyepoteza maisha na wengine kupata majiraha mwilini pamoja na dereva wa gari hilo. Kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa Morogoro katika  hospital ya mkoa Morogoro, baadae asubuhi mwili utaanza safari ya kuelekea Dar es Salaam.
IMG_4166IMG_4176 IMG_4213IMG_4214IMG_4215
Kweli ajuae mwisho wetu ni Mungu pekee. Tunaishi kama vile tunajua maisha yetu yataisha lini kumbe tunajidanganya. Haya matukio yote ni kwa ajili yetu kuamka na kujifunza kitu. Tumrudieni Mungu, tuungame dhambi zetu maana hakuna ajuae siku wala saa yake itakuwa lini. R.I.P Tyson na wote mliotutangulia.
Picha zote kutoka DJ Choka Music.

Msanii wa Hip Hop nchini, Ambwene Yessaya 'AY' (anayehesabu pesa) aliamua kujitole kununua jeneza la kusafirishia mwili w marehemu, jeneza hilo liligharimu kiasi cha shilingi laki sita ambazo AY alizitoa cash!
wakisaidiana kubeba jeneza hilo kuelekea hospitalini baada ya kulinunua
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba (mbele), akiongozana na AY kuelekea hospitalini
Mtangazaji wa kipindi cha Mboni Show, Mboni Masimba akilia kwa uchungu akiwa nje ya Hospitali ya Mkoa wa Morogoro wakati wakisubiri kusafirisha maiti kuelekea Dar. Marehemu Tyson ndiye alikuwa Mtayarishaji wa kipindi chake na walikuwa wote katika safari hiyo, ingawa walikuwa magari tofauti.
Mboni (kushoto) akiwa na Mtangazaji wa ITV, Devota Minja
Mboni akifarijiwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka.
(PICHA: Dastun Shekidele/GPL Morogoro)

Related posts

0 comments:

About the Author

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Pellentesque volutpat volutpat nibh nec posuere. Donec auctor arcut pretium consequat.

Proudly Powered by Blogger.