Discussion

...................................................

...................................................

...................................................

...................................................

kibongobongo mpango mzima

kibongobongo mpango mzima

PREZOO AENDELEA KUTHIBITISHA KWAMBA ANA HELA MBAYAAA, HIKI NDO ALICHOKIFANYA

Posted in
No comments
Sunday, June 1, 2014 By Unknown

pREZZOCMB

Baada ya story za hapa town kuzagaa kuwa Ommy dimpoz amefanya shopping ya maana huko majuu, ila ishu ilikuwa pale alipofanya matumizi ya viatu aina ya sneakers yaliyokuwa yanalingana na kipato(mshahara) cha mtu wa kati cha miezi mitatu hivi. hili jipya sasa kwa upande wa msanii wa kenya Prezzo baada ya kufanya kufuru zaidi. Hivi karibuni Prezzo ameonekana akivalia sneakers kutoka kwa designer maarufu wa kimataifa wa viatu ajulikanaye kama Christian Louboutin, viatu hivyo vina thamani ya shilingi milioni mbili = (2,000,000/-), viatu adimu kuvikuta kwenye maduka yetu haya ya kawaida ya kitaa, tukio lilowaacha mashabiki wengi mdomo wazi pale walipogundua haswa thamani halisi ya viatu hivyo.

Prezzo amezoeleka kuwa ni mtu wa matanuzi ya makubwa sana, kuanzia kubook private plane kuzunguka tu, kutoka mji mmoja hadi mwingine, kununua magari ya kifahari na mengine mengi ambayo kwa msanii wa kawaida imekuwa bado ni ndoto. Ila kwa msanii prezzo inasemekana utajiri wake si tu wa kutegemea muziki peke yake, mbali na muziki anafanya biashara nyingi tu, ikiwemo uuzaji wa madini.

Related posts

0 comments:

About the Author

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Pellentesque volutpat volutpat nibh nec posuere. Donec auctor arcut pretium consequat.

Proudly Powered by Blogger.