WACHINA WAKAMATWA NA SHEHENA YA MENO YA TEMBO BANDARINI DAR
Posted in
No comments
Wednesday, January 1, 2014 By Unknown
Wakuu,
Japo naiweka kama tetesi ila napenda ifahamike kuwa ukweli wake utajidhihiri muda si mrefu.
Tetesi yenyewe ni kuwa Kuna Wachina wamekamatwa na Shehena Kubwa ya Meno ya tembo Bandarini Dar na sasa wamechukuliwa kisiri na "watu flani" ambao hawataki habari hii ijulikane.
Napenda kuviarifu vyombo vyetu vya dola kuwa makini na "watu hawa flani" kwani wananchi hatutakaa kimya endapo hili litanyamaziwa.
Namna yoyote ya kuzima huu ujangili italeta balaa kubwa si kwa vyombo vya dola tu bali hata kuitia doa serikali kwa ujumla. Msifiche, waanike ili waueleze umma nani yupo nyuma yao!
Happy New Year 2014!
========
UPDATE:
Ili wajue tumeshajua na si siri na kiasi cha "mzigo" tunajua, naongeza data:
Ilikuwa ni meli ya kijeshi ya China ambayo ilikuwa imeegesha gati namba 3 baada ya kuwa nchini katika shughuli za kawaida za ushirikiano katika kudhibiti maharamia (Pirates). Katika kuuficha mzigo kwa kudai magari yamebeba chakula ndipo wakashtukiwa.
Chanzo chetu kinatufahamisha kuwa Wametiwa pingu na wanajeshi wa JWTZ na TISS na wamepelekwa Ukonga na msafara wa magari mawili yakiongozwa na pikipiki za Polisi.
Hata walipo tuna chanzo chetu ambacho kitaendelea kutujuza kinachojiri
Source: Jamii Forums
Related posts
Share this post
0 comments: