RAY C APATA NAFUU NA AMERUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI
Posted in
No comments
Wednesday, May 7, 2014 By Unknown
Mwanamuziki Rehema Chalamila ‘Ray C’, ametoka katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam alikokuwa amelazwa.
Mwanamuziki huyo ambaye amekuwa katika tiba ya kuachana na matumizi ya dawa za kulevya hospitalini hapo, alifikishwa hapo juzi Jumatatu asubuhi na baadhi ya madaktari walibainisha kuwa Ray C alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa dengue ambao umelipuka katika maeneo mengi jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Akizungumza kwa simu jana, Ray C alisema ameondoka hospitalini na yuko nyumbani baada ya kuruhusiwa na madaktari.
Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Sophinias Ngonyani alisema mwanamuziki huyo aliruhusiwa baada ya kupata nafuu na hali yake kuonekana nzuri.
Related posts
Share this post
0 comments: